Mamlaka ya mawasiliano nchini Uganda (UCC) imetoa amri ya kuvifungia vyombo vya habari 23 nchini humo kwa kukiuka maadali ya urushaji matangazo na kuzua taharuki kwa wamiliki.
Kwa mujibu wa msemaji wa UCC, Pamela Ankunda, amesema wamefikia uamuzi huo kufuatia Vituo hivyo kutangaza uganga wa kienyeji na kuwatapeli wananchi.’
Hatua hii inafuata onyo lililotolewa tangu zamani likiwasihi kuacha kuwaweka hewani waganga wa kienyeji.
“Kwa kuwaweka hewani matapeli wanaojiita waganga wa kinyeji, wakitumia mbinu mbalimbali wakiwa hewani ili kuwatepeli wananchi.”
“Kwa mfano kwa kuwalaghia wananchi kwamba ukituma fedha hizo kwa njia ya simu ya mkononi utapata utajiri, baada ya kutuma kesho yake utapata mamilioni ya fedha chini ya kitanda chako. Hivyo tumetumia sheria ya kuwajibisha radio hizo na kufunga FM Radio 23 baada ya kusikiliza matangazo hayo.” amesema Bi Ankunda.
Radio zilizofungiwa zimetajwa kuwa ni Metro FM, Nile FM, Kagadi Broadcasting Services, Emambya FM, Village Club FM, Radio Kitara, Packwach FM and Tropical FM,Apex FM, Bamboo FM, Ssebo FM, Eastern Voice FM, Eye FM, Victoria FM, RFM, Kiira FM, Tiger FM, Greater African Radio, Dana FM, Gold FM, Hits FM and Radio 5.
Mamlaka hiyo imerejea tangazo la umma lililotolewa 2014 Marchi, 27 ambapo vyombo vya habari vilipewa onyo kuacha kutangaza na kuhamasisha maswala ya kishirikina ikiwa ni kinyume na sheria ya urushaji matangazo nchini himo.
Ankunda amesema kuwa redio zitarudishwa hewani endapo tu zitakiri kufanya kosa hilo la kurusha vipindi hivyo vilivyohusisha ushirikina.
Na amezishauri stesheni za redio nchini humo kuwafundisha watangazaji wao juu ya maadili ya uandishi ili kuzuia kufanyika kwa makosa hayo.
Uganda inazaidi ya radio 270 zinazoruka kwenye masafa ya FM, kutokana na uchache wa matangazo inapelekea baadhi ya vituo vya redio kupokea aina yoyote ya tangazo ili kuingiza pesa za kuendesha vituo hivyo.