Maofisa nchini India wanachunguza ugonjwa ambao haujafahamika uliosababisha zaidi ya watu 140 katika mji wa Eluru huko Andhra Pradesh, nchini humo  kulazwa hospitali mwishoni mwa wiki hii.

Taarifa iliyotolewa na Daktari imeeleza kuwa wagonjwa hao wamekuwa na dalili za kichefuchefu na kukosa nguvu.

Maafisa wa afya wa hospitali ya Eluru wameiambia ‘The Indian Express’ “Watu wa India wanaugua, haswa watoto , ghafla tu wanaanza kutapita baada ya kulalamika kuwa macho yao yanawasha, wengine wanazimia au kukosa nguvu kabisa”.

Ugonjwa huo unakuja wakati India ikiwa inakabiliwa na mlipuko wa janga la Corona lakini vyombo vya habari vimeripoti kuwa wagonjwa hao walifanyiwa vipimo vya Corona na wote wakawa hawana na tayari hospitali hiyo imetenga vitanda kadhaa kwa ajili ya wagonjwa wa ugonjwa huo usiojulikana kama vitahitajika.

Wengi wao waliopelekwa hospitali wanaonekana kupona kwa haraka na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Waziri wa afya wa Andhra Pradesh Alla Kali Krishna Srinivas amesema sampuli za damu zao hazikuona ushaidi wowote wa maambukizi yatokanayo na virusi.

“Tunachunguza maji na hewa katika eneo ambalo watu wanaugua ugonjwa huo, Ugonjwa huu wa ajabu utadhibitika tu mara tu matokeo ya maabara yatakapotoka ,” amesema Srinivas.

Namungo FC kuikabili El Hilal El Obeid
Congo: Tshisekedi avunja ushirikiano na Kabila