Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewatoa hofu wakazi wa Wilaya ya Mbeya kutokana na kuwepo kwa taarifa ya uhaba wa mafuta katika baadhi ya Maeneo Mkoani humo.

Malisa aneyasema hayo, mara baada ya kutembelea katika baadhi vituo vya Mafuta Jijini Mbeya na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, huku akiambatana na Meneja wa wa EWURA Mkoa wa Mbeya, Dickson Semkuyu.

Katika ziara hiyo, Malisa amejionea hali halisi ya upatikanaji wa huduma ya mfuta na kubainisha kuwa hakutokuwa na Changamoto kubwa kuhusu uhaba wa mafuta.

Hata hivyo, amewataka Wafanyabishara, watumiaji wa Vyombo vya moto na Wakazi wa Mbeya kuwa watulivu wakati jitihada za dhati zikichukuliwa, ili kutatua changamoto hiyo.

Waliotega vilipuzi vya kienyeji Kanisani wadakwa
Aliyemwingilia Mgonjwa wa akili jela miaka 15