Naibu waziri wa kilimo maliasili mifugo nauvuvi, Dkt. Makame Ussi amesema Zanzibar ina uhaba wa rasilimali ya mchanga hivyo matumizi sahihi na matumizi yenye mpangilio yanahitajika kufanyika sasa.
Amesema umakini zaidi katika matumizi ya mchanga unahitajika kwasababu rasilimali hiyo ni kidogo huku matumizi yake kwa ujenzi wa nyumba na shughuli nyingine ukiendelea kufanyika kwa kiwango kikubwa.
Ametoa mfano hai kuwa ni maeneo ya mkoa wa kaskazini unguja pekee ndiyo yanayozalisha mchanga huku aridhi iliyobakia ikiwa ni udongo na jiwe huku baadhi ya mashimo yanayozalisha mchanga yamefungwa baada ya kuchibwa mchanga kinyume na utaratibu hadi maji yakaibuka.
” Yapo baadhi ya mashimo ya mchanga yameathirika vibaya kiasi ya kutoa maji chini ya ardhi kutokana na kuchimbwa mchanga bila kuzingatia viwango na utaratibu wake” amesema Dkt. Ussi
Amesisitiza kuwa Zanzibar ni kisiwa na juhudi za makusudi za uhifadhi wa mazingira zinahitajika ili kuepuka athari zinazoweza kukifanya kisiwa hicho kikatoweka.