Vyama vya Siasa 19 vilivyo na usajili na kudumu vitahakikiwa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ili kuangalia uhalali wao wa kushiriki

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amesema Vyama vitakavyoshindwa kukidhi vigezo havitashiriki Uchaguzi katika ngazi zote yaani Udiwani, Ubunge na Urais.

Ameongeza kuwa Ofisi yake inafanya zoezi la uhakiki mapema ili kutoa nafasi kwa Vyama kurekebisha dosari zozote ambazo zinaweza kuwazuia kushiriki Uchaguzi Mkuu

Jaji Mutungi amesema tayari wameshaandika barua kwa Vyama vyote na uhakiki huo utaanza rasmi Machi 10 mwaka huu

Aidha, ametoa wito kwa Vyama vya Siasa kutii Sheria bila shuruti wakati nchi ikielekea kwenye Uchaguzi.

Mfugale ''Kukatika daraja la kiyegeya kawaida lina miaka 40''
Viongozi wa Afrika washindwa kutwaa tuzo ya Mo Ibrahim