Lydia Mollel – Morogoro.

Jeshi la Polisi Mkoa Morogoro, limewataka raia wa kigeni waliopo Nchini kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali ikiwemo miradi ya Serikali, kutoa ushirikiano pale wanapoona viashiria vya vitendo vya kihalifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Alex Mkama ameyasema hayo alipotembelea mradi wa Bwawa la kuhifadhia maji la Vidunda lililopo Ngerengere, unaosimamiwa na Kampuni ya Sinohydro, Mkoani Morogoro.

Aidha, amewataka raia hao kutoa taarifa zote zenye viashiria vya kihalifu ikiwemo wizi na vitendo vyote vya kijinai, ambapo Msimamizi wa mradi huo Ma Ziheng amesema amefurahishwa na ugeni huo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, ili kuifanya Morogoro kuendelea kuwa shwari.

Ikumbukwe kuwa, utoaji wa taarifa za matukio ya kiuhalifu mapema, husaidia Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa haraka lakini pia kudhibiti matukio mengine yasiendele kutokea.

Vifaa Tiba, Noti bandia vyadakwa Njombe
Kaze anukia Ihefu FC