Dunia tayari imeadhimisha siku ya Kiswahili, huku ikitambua mchango wa lugha hiyo adhimu katika ukuzaji wa tamaduni, kujenga ufahamu na kukuza mjadala miongoni mwa jamii.

Akihutubia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan visiwani Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezihimiza balozi za Tanzania ambazo bado hazijaanzisha madarasa maalum ya kufundisha Kiswahili kushajiisha utumiaji wa lugha hiyo kwa usahihi.

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Rais Mwinyi alisema baadhi ya balozi tayari zimeazisha madarasa hayo na kutaka jitihada zaidi zifanyike kueneza Kiswahili huku Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo, Balozi Pindi Chana akisema historia inaonesha lugha ya Kiswahili imetumika katika ukombozi hivyo ni fahari kwa Tanzania kupewa hadhi ya kuwa na kituo cha urithi wa ukombozi wa Afrika.

Jumuiya Afrika Mashariki, yenyewe imeadhimisha siku ya Kiswahili jijini Kampala, Uganda, zikiandaliwa na Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, KAKAMA, kwa ushirikiano na wizara ya masuala ya Afrika Mashariki ya Uganda.

Kiswahili kinaimarisha mashirikiano ya uchumi, umoja na mahusiano ya kidiplomasia, huku matumizi ya lugha ya Kiswahili yakiendelea kushika kazi katika ngazi zote za serikali ikiwemo nyaraka mbali mbali pamoja na mihimili ya serikali kutumia lugha ya kiswahili.

Maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani yalianza Julai mosi kwa matembezi, kufanyika kwa midahalo Zanzibar na Tanzania bara, huku mataifa mengine katika Afrika pia yakihamasika kuadhimisha siku hii (Julai 7) iliyorasimishwa na Umoja wa Mataifa.

Hatimaye Mawaziri Tanzania, Zambia wakubaliana jambo
Maandamano kupinga ongezeko la kodi yaibua mvutano