Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametoa onyo kali kwa mahakama nchini humo akiitaka kuacha kuelemea upande wa upinzani kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha machafuko katika uchaguzi ujao.

Aidha, uchaguzi mkuu nchini  Kenya unatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao ambapo Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa umoja wa vyama vya upinzani NASA.

Kenyatta ameyasema hayo mara baada ya wapinzani kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya tume ya uchaguzi nchini humo kuhusu kupinga zoezi la uchapishaji wa karatasi za kupigia kura na kutaka zoezi hilo lisimamishwe mara moja.

Amesema kuwa mahakama haiwezi kuwa huru halafu ikatumia uhuru huo kuingilia Idara zingine za Serikali kwakuwa kila idara ina majukumu yake hivyo inapaswa kuyatekeleza kikamilifu.  

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Mahakama nchini humo, David Maraga amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kutoingilia mamlaka zilizowekwa kisheria ili kila mmoja apate haki yake ya msingi.

 

Hata hivyo, tume ya uchaguzi nchini humo inatarajia kukutana na wagombea wote wa kiti cha urais mapema hii leo akiwemo Rais Uhuru Kenyatta ili kuweza kupewa utaratibu maalum.

Alikiba Ft Davido 'Coming soon'
Video: Saa 72 hatma ya Lowassa Polisi, Mkapa afunguka