Kuelekea katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata kwa awamu ya pili, Serikali imechukua tahadhari na kuimarisha ulinzi katika mji huo ili kupisha shughuli nzima kumalizika salama bila ghasia yeyote.

Ambapo takriban viongozi 13 wa mataifa tofauti wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo, miongoni mwa viongozi wa kigeni wanaotarajiwa ni waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, rais wa Uganda, Yoweri Museveni na rais wa Rwanda Paul Kagame.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alisusia marudio ya uchaguzi ameitisha mkutano wa upinzani na amewataka wafuasi wake kususia sherehe hiyo na badala kuifanya siku hiyo kuwa siku ya kuwakumbuka wafuasi waliouawa katika ghasia.

Kufuatiwa na Uchaguzi wa mwezi Agosti uliofutwa na mahakama kutokana na kile kilichotajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki na kufanya marudio ya uchaguzi huo Oktoba 26 ulimpatia Uhuru Kenyatta asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa asilimia 39.

Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa jumanne ya Tarehe 28 Novemba, 2017, pia Naibu wa Rais, William Ruto anatarajiwa kuapishwa katika sherehe hiyo itayohudhuriwa takribani  na watu 60,000.

 

 

Video: Wabunge wamlima barua Spika, Haijapata kutokea
Nusu ya madiwani wa Mbowe wameomba kuhamia CCM- Polepole