Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amefanya mazungumzo na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini humo, Wafula Chebukati kabla ya uchaguzi wa marudio uliozua utata  nchini humo.

Kenyatta ambaye amekuwa akishinikizwa na wadau mbalimbali kukutana na afisa huyo pamoja na mgombea urais wa muungano wa NASA, Raila Odinga, ili kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea kuikabili nchi hiyo.

Aidha, baada ya mkutano huo, Kenyatta ametuma taarifa kwa vyombo vya habari iliyosema kuwa yeye hana masharti yoyote kwa tume hiyo, isipokwa tu kwamba uchaguzi ufanyike siku ya Alhamisi kama ilivyoagizwa na mahakama ya juu.

“Msimamo wangu ni ule ule, Wakenya wapewe nafasi ya kushiriki kwenye zoezi la kidemokrasia la kupiga kura kama tu ilivyoagizwa na mahakama ya juu. hatuna masharti yoyote kwa IEBC,” amesema Kenyatta

Hata hivyo, kwa upande wake, Kiongozi wa muungano wa NASA ameendelea na mikutano ya hadhara katika kaunti ya Kisii na kuwataka wafuasi wake kutoshiriki kwenye uchaguzi huo wa Alhamisi

Video: Daktari Muhimbili aeleza jinsi kope za bandia zinavyosababisha upofu
Video: Lulu akana kusababisha kifo cha Kanumba, Uteuzi wa Gavana mpya watikisa