Mshambuluaji wa Mwadui FC Uhuru Seleman Mwambungu amesema ana siri moyoni mwake kuelekea msimu ujao wa 2021-21.

Uhuru amesema hayo alipozungumza na Azam TV baada ya mchezo wa 33 wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Uhuru amesema siri hiyo huenda akaifichua baada ya michezo ya mwisho ya Ligi Kuu itakayochezwa Jumapili Julai 18.

“Watanzania wanapenda sana kudharau wachezaji wao, nina jambo moyoni mwangu litafahamika baada ya mchezo wa mwisho”

Kuhusu kuendelea na Mwadui FC iliyoshuka daraja msimu huu, Uhuru amesema suala hilo nalo litafahamika baada ya mipango yake kama ataendelea kuwepo klabuni hapo ama kuondoka.

Amesema kazi yake ni kucheza soka hivyo lolote litakalokuwa atakubaliana nalo.

“Mipango yangu ni kucheza mpira kama itashindikana kucheza Ligi Kuu nitaendelea na Mwadui FC katika michuano ya Ligi Daraja la kwanza.”

Katika mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union, Mwadui FC imefungwa mabao 5-0.

Rais Samia kushiriki maonyesho ya kimataifa Dubai
TRC yatia saini mkataba ununuzi wa vichwa 17 vya treni