Uingereza leo imeidhinisha matumizi ya jumla ya chanjo ya Covid-19 na kutangaza uzinduzi wa dawa ya kampuni ya Pfizer-BioNTech kuanzia wiki ijayo.

Waziri wa Afya Matt Hancock amethibitisha hilo wakati wizara yake ikitangaza idhini ya matumizi ya dharura kutoka kwa Shirika la Uingereza la Udhibiti wa madawa na bidhaa za afya.

Hancock amesema Uingereza itakuwa nchi ya kwanza duniani kuidhinisha matumizi ya jumla ya chanjo hiyo, akiongeza kuwa dozi za mwanzo 800,000 zitatolewa.

Wizara ya Afya imesema makundi ya kipaumbele kupewa chanjo hiyo yatajumuisha watu wanaoishi katika makazi ya wazee na walemavu, wahudumu wa afya, wazee na watu walio katika hatari kubwa.

Uingereza inakuwa nchi ya kwanza ya magharibi kuidhinisha chanjo ya Covid-19 hii ikiwa ni hatua ya kihistoria ya juhudi za kupambana na virusi vya corona.

Msola: Mchakato wa mabadiliko umepiga hatua kubwa
Ndala: Tunakwenda Tanzania kuishangaza dunia