Imeripotiwa kuwa mdogo wake Kim KardashianKylie Jenner ni mjamzito na anatarajia kupata mtoto na mpezi wake mpya rapa Travis Scott.

Kylie mwenye umri wa miaka 20 aliwahi kuwa katika mahusiano na nyota wa hiphop Micheal Ray Stevenson maarufu kama ‘Tyga’ kabla ya kuachana mapema mwezi Aprili.

Baada ya mtandao wa TMZ kuripoti kuwa Kylie ana ujauzito wa miezi minne Tyga ameibuka na kudai mtoto ni wake jambo ambalo limewashanagaza wengi katika mitandao ya kijamii.

Tyga aliposti ujumbe kwenye mtandao wa Snapchart akisema mtoto ni wake  “that’s my kid”, ujumbe amabao badae aliufuta.

Kylie kwa sasa yuko na Tavis Scott baada ya kuachana na Tyga na mrembo huyo alisema hakuachana na Tyga kwa ugomvi bali makubaliano ya amani tu na hawana ugomvi wowote.

 

 

Video: Atletico Madrid yaibamiza Sevilla
Video: TCRA yazindua Kampeni 'Usinitumie, Sitaki, Situmii wengine, nitakuripoti'.