Serikali imejenga jumla ya kilomita 317.65 za barabara kwa kiwango cha lami ambazo zimehusisha barabara kuu, barabara za mikoa na wilaya, ujenzi ambao umesaidia kurahisisha utoaji wa huduma ya usafiri na usafirishaji katika maeneo tofauti nchini ukizingatia uendelevu kwa watumiaji wa sasa na wa baadaye.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dodoma kupitia Hotuba aliyoitoa Bungeni nakuongeza kuwa, Serikali pia inatambua umuhimu wa kupunguza msongamano wa magari katika majiji na miji, ili kuongeza ufanisi katika utendaji nautekelezaji wa majukumu ya wananchi na ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Amesema, katika hatua za kuhakikisha kuwa huduma za uchukuzi zinaboreshwa, Serikali inaendelea na awamu ya Pili, Tatu, Nne na Tano ya ujenzi wa barabara na Miundombinu ya Mabasi yaendayo
Haraka Mkoani Dar es Salaam na ujenzi wa barabara za mchepuo (bypass) katika Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Maswa.
“Awamu ya Pili (BRT II) ya ujenzi inayohusisha barabara ya Kilwa toka katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuelekea Mbagala na barabara ya Kawawa kutoka makutano ya Magomeni kupitia Chang’ombe hadi makutano ya barabara ya Kilwa umefikia asilimia 82. Mradi huu una barabara zenye urefu wa kilomita 20.3; vituo vya mabasi 29; barabara za juu mbili; majengo mawili ya Terminal; Depot moja na Feeder station nne.” amesema Waziri Mkuu.
Aidha, ameongeza kuwa, awamu ya Tatu (BRT III) inayohusisha Barabara ya Nyerere kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam hadi Gongolamboto yenye urefu wa kilomita 23.6 imekamilika kwa
asilimia 5.