Mradi wa bwawa la umwagiliaji lililopo eneo la Msagali na Chunyu Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, lenye uwezo wa kuzalisha lita trilioni 90 za maji na ujenzi wake kugharimu shilingi 27 Bilioni, umekabidhiwa rasmi kwa Mkandarasi ili uanze kutekelezwa kwa ajili ya kusaidia ukuzaji wa sekta ya kilimo.
Akikabidhi mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amemtaka Mkandarasi huyo kutekeleza jukumu lililo mbele yake kwa wakati ili kufanikisha dhana ya Rais ya kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo.
Kufuatia hatua hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mwalimu Josephat Maganga amewataka Wananchi kuepuka uuzaji holela wa ardhi, ili kuepuka uzalishaji wa migogoro.
Awali, wakiongea katia eneo hilo, watekelezaji wa mradi huo mhandisi mkoa wa Dodoma, Raphael Raizer na mhandisi wa mradi, Emmanuel Mponda wameainisha maeneo muhimu ambayo wanatarajia kuyakamilisha wakati wa utekelezaji wake.
Mradi wa bwawa la umwagiliaji la Msagali na Chunyu unaoanza Oktoba 2022, unatarajia kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya kilimo kwa wananchi wilaya ya Mpwapwa mara bada ya kukamilika kwake Machi,2024 na litakuwa na uwezo wa kuzalisha lita za maji zipatazo trilioni 90.