Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo ameiagiza Serikali Mkoani Rukwa pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kutuma timu ya uchunguzi ili kubaini kinachokwamisha Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini kukamilika, huku ukionekana kutekelezwa chini ya kiwango cha ubora na thamani ya fedha kilichopelekewa hadi sasa.

Chongolo ameyasema hayo baada ya kutoridhishwa na ujenzi huo na kukerwa na mkandarasi wa Mradi wa Maji wa Ilemba, Jimbo la Kwela, ambaye pamoja na RUWASA Mkoa wa Rukwa kumwekea msukumo, ili ajenge kwa kasi ya kukamilisha ndani ya muda wa mkataba, bado ameendelea kusuasua.

Amesema, “Mkuu wa Wilaya, hakuna kucheka na waliopewa kazi hizi. Tukiacha hali hii, mambo hayataenda na hiyo sio sawa hata kidogo. Hatuwezi kuacha mambo yaende namna hii. Tutakuwa hatutendi haki na tutakuwa hatujitendei haki wenyewe na nafasi zetu za kuwatumikia wananchi. Wananchi wanachotaka ni huduma”.

Komredi Chongolo alitoa maelekezo hayo Oktoba 10, 2023 akiwa katika Kata ya Mtowisa na Ilemba, mara baada ya kukagua mradi huo wa Maji wa Ilembo wa Tsh. 1.9 bilioni ambao bado uko asilimia 27 na hospitali ya wilaya iliyoanza kujengwa tangu Disemba 2021 na mkandarasi aitwae Kuyella Enterprises, huku ukitakiwa kukamilika Machi 2022, lakini hadi alipofika mahali hapo kuutembelea na kuukagua, ulikuwa haujakamilika.

Simba SC, Young Africans zarudiwa Kwa Mkapa
Tanzania kufanya mageuzi kiuchumi - Rais Samia