Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, umefika asilimia 50 na kutumia takriban Bilioni Saba mpaka sasa tangu kuanza kwake Oktoba 2021 na ukitarajiwa kukamilika Oktoba 2023.
Kaimu Katibu Mkuu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu amesema jijini Dodoma, nakuongeza kuwa Serikali inatoa fedha kwa wakati kwa Mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kulingana na Mkataba.
Amesema, “Eneo letu Lina ekari 7, na Jengo hili linalojengwa hapa litakua na ghorofa 6 ambazo zitajumuisha Ofisi za Idara na Vitengo, ofisi za viongozi, Kumbi za Mikutano pamoja na maeneo ya bustani na viwanja vidogo vya michezo.”
Kuhusu upande wa Mkandarasi, Msimamizi wa Jengo hilo Omari Chitawala amesema ujenzi unazingatia masharti yote ya Mkataba ikiwemo ubora na viwango vinavyotambulika.