Serikali ya Ujerumani kupitia kwa Balozi wake Nchini Tanzania, Dkt. Detlef Waechter imetiliana saini ya ufadhili na Taasisi ya Busara Promotions waandaaji wa tamasha la Sauti za Busara linalofanyika kila mwaka visiwani Zanzibar.
Ujerumani imekubali kuchangia fedha ambazo zitaenda kufanikisha shughuli za tamasha hilo msimu wa 16, mwaka 2019.
Hafla hiyo imefanyika Oktoba 18, 2018 katika ofisi za Ubalozi huo Jijini Dar es Salaam.
Aidha, tukio hilo la kutiliana saini, limewahusisha Balozi huyo wa Ujerumani nchini Dkt. Detlef Waechter pamoja na Mwenyekiti wa Tamasha hilo la Sauti za Busara, Simai Mohammed Said ambaye pia (Mwakilishi wa jimbo la Tunguu).
Ufadhili huo ni juhudi za Wizara ya Mambo ya Nje ya nchini Ujerumani katika kuunga mkono utamaduni wa Tanzania kwa kufadhili Tamasha hilo la kimataifa la Muziki ambalo limekuwa pia kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi visiwani Zanzibar.
Kwa upande wake Balozi Dkt. Detlef Waechter amemhakikishia Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza utamaduni wa Mtanzania kwa kuongeza fursa na tija zitokanazo na zao la ushirikiano wa Nchi hizo mbili.
Naye mwakilishi wa Busara Promotions amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo lenye kauli mbiu “Where African Music Stars Shine Brightly”, yanaendelea na tayari wamechapisha majina ya Wasanii na bendi pamoja na Nchi wanazotoka miongoni mwao ni Staa wa muziki wa Hip Hop, Fareed Kubanda maarufu kama “Fid Q” kutoka Tanzania.
Pia wapo: Mokoomba (Zimbabwe), Afrigo Band (Uganda), Fadhilee Itulya (Kenya), Ifrikya Spirit (Algeria), Rajab Suleiman & Kithara ( Zanzibar), Tune Recreation Committee, (Afrika Kusini), Ithrene (Algeria).
Wengine ni: Hoba Hoba Spirit (Morocco), M’Toro Chamou (Mayotte/Reunion), Trio Kazanchis +2 (Ethiopia/Switzerland), Faith Mussa (Malawi), Shamsi Music (Kenya), Sofaz (Reunion), Dago Roots( Reunion), Lydol (Cameroun), Jackie Akello (Uganda).
Wamo pia: S Kide & Wakupeti Band (Tanzania), Tausi Women’s Taarab (Zanzibar), Mkubwa na Wanawe Crew (Tanzania), Damian Soul (Tanzania) na Wamwiduka Band (Tanzania).
-
Video: JPM akutana na Taifa Stars Ikulu, akabidhi milioni 50
-
Mahakama yapiga chini pingamizi la matokeo ya urais
-
Marekani yaipongeza Tanzania kwa kuvutia wawekezaji
Tamasha hilo la 16 litafanyika Mji Mkongwe Zanzibar kuanzia tarehe 7 – 10 February 2019 huku majukuwaa 3 tofauti yatawaka moto kwa muziki wa moja kwa moja ‘live’ kwa muda wa siku zote za tamasha kuanzia asubuhi, mchana na Usiku.