Vyama vya kihafidhina vya upande wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na kile cha Social Democratic (SPD) vimekubaliana kuunda serikali ya pamoja,
Vyama vya Ujerumani vilivyopo katika mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto vimeweza kuafikiana juu ya nafasi mbalimbali za mawaziri, lakini bado vinaendelea na mazungumzo kupata makubaliano ya mwisho.
Aidha, Kulingana na shirika la habari la dpa pamoja na gazeti la Ujerumani la Bild, chama cha SPD kitachukua wizara tatu za juu – wizara ya mambo ya nje, wizara ya fedha na wizara ya ajira na ustawi wa jamii katika serikali mpya ya mseto ya Ujerumani. huku chama cha Merkel cha Christian Democratic Union (CDU) kikichukua wizara ya uchumi pamoja na ya ulinzi.
Hata hivyo, mpango wowote utakaofikiwa utahitaji kuidhinishwa na wanachama 464,000 wa chama cha SPD, ambao watalazimika kuupigia kura ya posta kabla ya chama hicho kuchukua hatua ya kuunda muungano mwengine tena na vyama vya Merkel baada ya kuwa mshirika wake mdogo tokea mwaka 2013.
-
Aliyesimamia kuapishwa kwa Raila ashtakiwa kwa uhaini
-
Mpango wa Trump kuboresha nyuklia walaaniwa vikali
-
Dada yake Kim Jong Un kuhudhuria Olympics Korea Kusini
Baada ya hapo Merkel atakuwa na mamlaka ya kuteua baraza la mawaziri na vyama hivyo vitasaini mkataba wa serikali ya muungano.