Mgombea wa Ukansela wa vyama vya muungano wa kihafidhina vya CDU na CSU nchini Ujerumani, Armin Laschet anakabiliwa na mvutano unaoendelea ndani ya chama chake baada ya kushindwa katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili.

Wakati Laschet na viongozi wa vyama vingine wakikutana kuamua hatua zijazo za kuchukua, wito umekuwa ukitolewa kumtaka Laschet akubali kuwa ameshindwa na ajiuzulu.

Kwa mujibu wa DW akizungumza jana usiku, baada ya kukutana na kundi la wabunge wapya wa CDU na CSU, Laschet amesema anapanga kufanya mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano na chama cha Kijani na FDP. Kiongozi wa CSU, Markus Soeder amesema kiongozi wa chama cha SPD, Olaf Scholz ana nafasi nzuri ya kuwa kansela na kumrithi Angela Merkel.

SPD, imesema tayari imevialika vyama vya Kijani na FDP kwa mazungumzo wiki hii. Jana Scholz aliwahutubia wabunge wapya wa chama chake kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Biashara United walamba Milioni 10
Mo Dewji akasimu madaraka Simba SC