Wanasiasa nchini Ujerumani leo wameanza juhudi za kuunda serikali mpya baada chama cha SPD kupata ushindi katika uchaguzi uliofanyika jana.
Viongozi wa vyama vilivyopata nafasi ya kuingia Bungeni wamekutana kutathmini matokeo ya uchaguzi wa shirikisho ambao umeshindwa kutoa mwelekeo kamili wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya.
Mgombea wa Ukansela kupitia chama cha SPD kilichojikingia asilimia 25.9 ya kura Olaf Scholz amejisifia kuwa anaweza kuunda serikali inayokuja.
Katika uchaguzi huo wa jana vyama ndugu vya kihafidhina vya CDU/CSU vimepata asilimia 24.1 ya kura na kufuatiwa na chama cha kijani kilichopata asilimia 14.8.
Kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi SPD na mgombea wake Franziska Giffey kimepata asilimia 21.4 ya kura na kukipiku chama cha walinzi wa mazingira kilichojikingia asilimia 18.9 ya kura.