Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas anafanyakazi ya kunusuru makubaliano ya nyuklia ya Iran, huku Marekani ikitishia vita katika Ghuba ya Uajemi.

Heiko Maas anajaribu kuishawishi Iran kutojitoa katika makubaliano yanayojulikana kama Mpango Mpana wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPAOA), ulioanza kutekelezwa Julai 7. 2015 kufuatia majadiliano magumu na mataifa ya Ulaya.

Marekani inaituhumu Iran kuwa inapanga mashambulizi dhidi ya maeneo ya Marekani katika kanda hiyo na kuituhumu kwa kuhusika na mashambulizi dhidi ya meli nne za mafuta nje ya pwani ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Aidha, katika muda wa miezi kadhaa iliyopita, utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump umeimarisha vikwazo vyake dhidi ya Iran kama sehemu ya kampeni yake ya shinikizo la juu kabisa.

Hata hivyo, malengo makuu ya ziara ya Maas ni kuzifanya Marekani na Iran kushiriki mazungumzo ya moja kwa moja lakini hilo halitatokea bila ya Marekani kuondoa baadhi ya vikwazo vyake.

 

 

LIVE: Yanayojiri Bungeni jijini Dodoma leo Juni 10, 2019
Watu wanne waripotiwa kuuawa nchini Sudan

Comments

comments