Kasi ya Maendeleo na kupambana na ufisadi unayooneshwa  na Rais John Magufuli imeendelea kuvuta usikivu wa Mataifa mbalimbali ambayo yameanza kumsifia.

Serikali ya Ujerumani kupitia Mkurugenzi wake wa Afrika, Wizara ya mambo ya nje, George Schmidt impongeza rais Magufuli na kueleza kuwa mapambano aliyoyaanzisha dhidi ya rushwa kwa vitendo yatailetea maendeleo makubwa Tanzania.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Schmidt alisema kuwa serikali ya Ujerumani itashirikiana kwa karibu na Magufuli katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Alisema kuwa Ujerumani imeona fedha zilizokuwa zinatumika kiubadhirifu sasa zitatumika kwa maendeleo ya taifa kama ilivyokusudiwa.

Kiongozi huyo yuko nchini kwa ajili ya ziara ya siku tano yenye lengo la kuangalia maendeleo baada ya uchaguzi Mkuu.

Ufafanuzi Kuhusu Serena Hotel Kufungwa Kwa Kukwepa Kodi
Mshike Mshike Wa SDL Kuendelea