Ujerumani imewataka wahamiaji ambao maombi yao ya kupata hifadhi yamekataliwa kuondoka nchini humo kwa hiari na kurejea kwenye nchi wanazotoka pia wanaweza kupewa msaada wa kifedha.
Hayo yamesema na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Thomas de Maiziere wakati akizungumza na gazeti la Bild am Sonntag, ambapo amesema kuwa mpango huo ni kwa ajili ya kuwasaidia wahamiaji hao pindi watakaporejea nchini mwao.
Aidha, nchi hiyo imekuwa ikitoa msaada wa fedha kwa wahamiaji wote waliokataliwa kupewa hifadhi ili kuwasaidia waweze kurejea kwenye nchi zao, zikiwemo gharama zinazohusiana na safari pamoja na fedha za kuanzia maisha pindi watakaporejea.
“Wakiamua kurejea nyumbani kwa hiari ifikapo muda ambao serikali imeupanga, tutawasaidia fedha za kuwarejesha makwao na kuanzia maisha katika nchi zao,”amesema de Maiziere.
-
Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefu
-
Maaskofu watoa ya moyoni kuhusu Rais
-
Ujerumani yatoa fedha kuwasaidia wakimbizi waishio Tanzania na Rwanda
Hata hivyo, Shirika la Ujerumani linalohusika na kuwasaidia wakimbizi, Pro Asyl, limeukosoa mpango huo likisema ni mkakati usio na manufaa na sio wa kuaminika, huku Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Guenter Burkhardt, akisema kuwa serikali inajaribu kuwashawishi watu kuacha kuzitetea haki zao bila ya kupata msaada.