Aprili 8 mwaka huu ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kwa marehemu Reginald Abraham Mengi ambaye ni bilionea na mfanyibiashara mkubwa nchini Tanzania kuchapisha ujumbe wa mahaba kwa mkewe Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi katika mtandao wa Twitter.

Kupitia ukurasa wake amekuwa akiandika jumbe zilizokuwa zikigusa hisia za watu wengi zaidi ambao wamekuwa wakiyatamani maisha ya mahusiano ya wawili hao.

Kupitia Twitter aliandika;

”JNMengi, my sweetheart, I love you more than the sand in all the seas in the whole world. God willing will see you tomorrow”

Akimaanisha anampenda sana mpenzi wake Jacqueline zaidi ya idadi ya mchanga uliopo bahari zote duniani na kumalizia kuwa wataonana kesho.

Huo ndio ulikuwa ujumbe wa mwisho marehemu Mengi kuandika juu ya hisia kali alizonazo kwa mke wake Jackline Ntuyabaliwe aliyemzalia mapacha wawili.

Mbali na ujumbe huo Post ya mwisho ya Mengi amezungumza juu ya urafiki na biashara akimnukuu Bilionea wa zamani wa Marekani John D, Rockefeller.

Ambapo aliandika

”Urafiki unaotokana na biashara zenu ni bora kuliko biashara itakayozaliwa kutokana na urafiki wenu” Billionea wa zamani wa Marekani John D,Rockefeller”.

Huo ndio ujumbe wake wa mwisho kwa watanzania katika kujenga mafanikio yao ambapo yeye aliamini katika falsafa hiyo.

Aidha, Dk. Mengi amefariki dunia usiku wa Mei 2, 2019.

 

 

Bobi Wine aachiwa kwa dhamana, akamatwa tena
Bunge laomboleza kifo cha Dr. Mengi