Waziri Mkuu wa Uingereza, Liz Truss ametangaza kujiuzulu baada ya wiki kadhaa za ukosoaji kutoka kwa wapinzani wake na wanachama wa chama chake cha Conservative, akiungana na wateule wake wawili wakuu katika baraza la mawaziri ambao nao wameachia ngazi.
Truss ametangaza kujiuzulu nje ya makazi yake jijini London, muda mfupi uliopita hii leo Oktoba 20, 2022 huku akisema atasalia kama Waziri Mkuu hadi mrithi wake atakapochaguliwa, katika uchaguzi wa viongozi utakaokamilika ndani ya wiki ijayo.
Liz Truss, aliingia madarakani wakati wa matatizo makubwa ya kiuchumi na alichaguliwa akiwa na mamlaka ya mabadiliko lakini, aliwahi kusema kwamba, “Natambua ingawa siwezi kutekeleza mamlaka.”
Liz amehudumu katika nafasi hiyo kwa wiki sita pekee, akiwa ni mmoja wa wasimamizi waliohudumu kwa muda mfupi zaidi katika historia ya kisiasa ya Uingereza huku kukiwa na mfululizo wa makosa na maono ya mengi ya kisiasa yalikataliwa baada ya athari mbaya ya masoko ya fedha.
Akishirikiana na mshirika wake wa kisiasa, Kwasi Kwarteng, Truss alikuwa ameingia ofisini akiahidi kupunguza kodi na kuanzisha ukuaji wa uchumi wa nchi, lakini wakati Kwarteng alipotangaza punguzo kubwa la kodi bungeni, sambamba na mipango mipya ya matumizi inayolenga kulinda kaya kutokana na bei ya juu ya nishati, sarafu ya nchi hiyo ilishuka thamani na deni la Serikali kupaa.