Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameonyesha kukasirishwa na utaratibu usiofaa wa ukamataji wa magari kwenye maegesho yasiyo rasmi “wrong parking” ambapo ameelekeza kuhitishwa kikao Cha pamoja baina yake, Wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA ili kupatia ufumbuzi Jambo hilo.

RC Makalla amefikia hatua hiyo baada ya kupokea Malalamiko mengi ya Wananchi juu ya utaratibu mbovu unaotumika na kusema Kama kiongozi hawezi kuruhusu Jambo hilo liendelee.

Aidha RC Makalla amesema amebaini pia baadhi ya vijana wanaofanya kazi hiyo wamekosa weledi na busara na wengi wao wamekuwa wakivizia mtu afanye kosa ili wamuadhibu badala ya kutoa elimu ili makosa yasifanyike.

Mheshimiwa Makalla amesema hayo wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Jengo la utawala la Manispaa ya Ubungo ambapo ameipongeza Manispaa hiyo kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na kuwataka Watumishi kutoa huduma Bora kwa wabanchi.

Hata hivyo RC Makalla ameipongeza Manispaa hiyo kwa ukusanyaji Mapato Jambo linalopelekea waanze kutekeleza miradi kwa Fedha za ndani na pia kutumia Force akaunti kukamilisha miradi iliyokuwa ikisuasua ikiwemo Jengo hilo la utawala.

Mitungi zaidi ya gase inahitajika - Prof. Masenga
Kanye West, Jay Z kwenye albamu moja