Mito ya Ulaya, yenye njaa ya maji na inayokabiliwa na ukame, imefichua mabaki ya meli zinazosadikika kupata ajali, ikiwemo kuonekana kwa masalia ya vitu mbalimbali na mabomu.
Moja ya mito hiyo ni Danube ambao unapungua maji kwa kasi ambapo hivi karibuni mabaki ya meli za kivita za Ujerumani za zaidi ya 12 zilizozama mwaka 1944, yameibuka na kuweka uwezekano wa kuhatarisha boti zingine kupata ajali.
Nchini Italia, msingi wa daraja la miaka 2,000 huko Roma uliibuka kwenye mto Tiber, wakati wavuvi walipopata bomu la kilo 450 katika Mto Po huku nchini Uhispania, mnara wa megalithic wa milenia nne hadi tano uliinuka karibu na jiji la Madrid.
Aidha, uwepo wa joto kali umedhoofisha uwezo wa Ulaya wa kuunda usambazaji wake wa nishati kwa kupunguza nguvu ya maji nchini Norway, kutishia vinu vya nyuklia nchini Ufaransa, na kusababisha vikwazo.
Kwa upande wa Uingereza, yenyewe ilipiga marufuku matumizi ya mabomba ya nje baada ya kukumbwa na ukame zaidi mwezi wa Julai tangu 1935, wakati baadhi ya miji ya Uhispania imezuia matumizi ya maji.
Ukame huo, umesababisha hofu katika bara zima, ambapo mawimbi ya joto yanaongezeka mara kwa mara yakiwa na nguvu zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya sayari ya Dunia na inaarifiwa ongezeko la joto duniani lina jukumu kubwa.
Kinachojulikana kama mawe ya njaa pia yameibuka tena, ambayo yana michoro ya miaka ya nyuma inayosomeka “Ukiniona, lia” na hii ni baada ya viwango vya maji kupungua, na wakazi wa eneo hilo walijua mavuno yangekuwa mabaya na mwaka uliofuata ulikuwa mgumu ikiwemo katika nchi za Jamhuri ya Cheki.