Shirika la Waandishi Wasio na Mipaka (RSF), limesema ukandamizaji unaofanywa na Iran dhidi ya waandamanaji umechangia kuongeza idadi ya waandishi habari waliofungwa jela hadi kufikia 533 katika mwaka wa 2022 ulimwenguni.

Idadi hiyo, imepanda kutoka Waandishi 488 katika mwaka wa 2021 huku zaidi ya nusu ya idadi hiyo wanazuiliwa katika nchi tano pekee ambazo ni China, inayoongoza ulimwenguni kwa kuwafunga waandishi ikiwa na 110, ikifuatwa na Myanmar 62, Iran 47, Vietnam 39 na Belarus 31.

Wanahabari wakiwa katika kazini. Picha ya N.News

Katibu Mkuu wa RSF, Christophe Deloire amesema katika taarifa yake kuwa tawala za kiimla na za kimabavu zinajaza magereza mengi kwa kasi, kuliko wakati mwingine kutokana na kuwafunga waandishi wa habari.

Amesema, hali hiyo inadhihirisha kuwa ipo haja ya dharura ya kuzipinga serikali zinazotekeleza vitendo hivyo na kuonyesha mshikamano na wale wote wanaounga mkono uhuru wa wanahabari na vyombo vya Habari.

Baiskeli chanzo kifo cha Mwandishi Kilimanjaro
Nabi: Nafasi ya Robo Fainali ipo wazi