Chama Cha United Democratic Party (UDP), kimesema kuwa hakitakuwa na mikutano ya hadhara ya Kampeni na badala yake watapita nyumba kwa nyumba kuwasilisha sera zao.

Naibu Katibu Mkuu wa UDP, Juma Khamis Faki, amesema Chama chao kwa sasa kinakabiliwa na ukata mkubwa wa fedha, hivyo wameshindwa kufanya mikutano ya hadhara ya Kampeni zao.


Faki amesema kuwa pamoja na kuikosa mikutano ya Kampeni, wameona kupita nyumba kwa nyumba ni njia rahisi ya kuwafikia walengwa katika kuwaomba kura.

UDP inaingia katika orodha ya vyama ambavyo tayari vimesitisha kampeni za uchaguzi mkuu ikiwa ni pamoja na Vyama vya NCCR  – Mageuzi, Alliance for African Farmers (AAFP), Sauti ya Umma (SAU) na Democratic Party(DP) vikilalamikia ukata wa Fedha.

Kenya: Wanafunzi wenye mimba waruhusiwa kurudi Shule
Lipumba kuboresha mfumo wa fedha

Comments

comments