Abel Paul, Jeshi la Polisi – Arusha.
Mtaandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha, umesema elimu zaidi itasaidia kuibadilisha jamii ya watanzania katika kukabiliana na vitendo vya ukatili vinavyotokea katika maeneo tofauti tofauti huku likibainisha kuwa litaendelea kutoa elimu ili kubadilisha fikra potofu kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Mtaandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha TPF-Net, Mrakibu Msadizi wa Polisi Jane Magesa wakati akitoa elimu katika Kituo cha Nyumba Salama ya Amani Arusha, kutokana na kutokuelewa kwa wananchi juu ya ukatili wa kijinsia.
Amesema, TPF-net Mkoa wa Arusha itaendelea kutoa elimu ili kuifanya jamii kuendelea kuwa salama na kuepuka kutenda vitendo vya ukatili huku akiwataka wanawanchi kuendelea kukemea vikali tabaia ya baadhi ya watu wachache wanaofanya vitendo hivyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Arusha, Mkaguzi msadizi wa Polisi Urusula Mosha amewahimiza wananchi wananchi kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili kwa Jeshi la Polisi huku akiwataka pia kutumia nyumba za ibada kutoa taarifa hizo za vitendo vya ukatili ili ziwafikie kwa haraka na kuzifanyia kazi.
NaYe Mlezi wa kituo cha Nyumba Salama ya amani Arusha mbali na kupongeza mtaandao wa Polisi wanawake TPF- net Mkoa wa Arusha amewaomba Jeshi hilo kuto ishia kituo hicho kutoa elimu wafike pia katika makundi mengine ya wahanga wa ukatili na kutoa elimu kwa wananchi ili kujenga jamii yenye uelewa mpakana juu ya vitendo vya ukatili.