Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili Nchini, Dawati la Jinsia na watoto Mkoani wa Ruvuma likiongozwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Odillia Mroso na Kamati ya Kupinga ukatili Mkoani humo wametembelea kaya za waathirika wa ugonjwa wa Ukoma ambao wamesema wamefarijika.

Kaya hizo, ni zile zilizopo Halmashauri ya Songea Vijiji, katika Kata ya Litisha na vijiji vya Morogoro, Magima na Litisha ambapo wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa waathirika wa ugonjwa huo, walio chini ya Uongozi wa Shirika la Masista Wabenedictini Peramiho.

Katika msaada huo waathiriwa hao walipatiwa Vitu mbalimbali ikiwemo Sabuni, Mafuta ya kula na kupaka, Mchele, Unga, Chumvi, Sukari, Soda, Nguo kwa Wahanga hao wa jinsia zote ambapo Vitu vyote vina thamani ya shilingi Milioni Moja.

Akipokea misaada hiyo, Sista Daniela Ngonyani ambae ni Msimamizi wa Kituo hicho alilishukuru Jeshi la Polisi na Wadau kwa kuguswa na kuamua kuungana kwa pamoja kutembelea waathiriwa hao na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali ambapo inekuwa faraja kwake na wahitaji hao.

Kwa upande wao Waathiriwa wa ugonjwa huo wa Ukoma walishukuru ujio wa Jeshi la Polisi na wadau hao na kusema wamefarijika na msaada waliopatiwa utawasaidia kujitimizia mahitaji yao na kutatua changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili.

Picha: Rais Samia katika maadhimisho Miaka 62 ya Uhuru
Magari ya kifahari yatumika usafirishaji Dawa za kulevya