Mkaguzi Kata wa Kata ya Makuro, ambaye pia ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Balumu Saguda amesema wahanga wakubwa wa ukatili wa kijinsia ni Wanawake, Watoto na watu wenye Ulemavu.

Balumu ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa elimu ya ushirikishwaji jamii, kwenye Mahafali ya kuhitimu elimu katika Shule ya Msingi ya Seminari Diagwa, iliyopo Kata Makuro, Tarafa ya Mtinko Wilaya na Mkoa wa Singida.

Amesema, wahitimu wanatakiwa kutimia njia sahihi za kutoa taarifa pindi wanapotendewa au kuona dalili za ukatili wa kijinsia, kwa viongozi wa Serikali za Mitaa na Jeshi la Polisi ili wahusika wakamatwe na kufikishwa Mahakamani.

Awali, Padri Girbert Mwiru aliwataka wazazi kuwalinda watoto na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, kwani ikitumika vibaya inachangia kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili, ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.

Waumini saba wauawa Msikitini, watatu majeruhi
Wakaguzi wa Polisi watakiwa kutumikia viapo vyao