Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa, umeeleza kuwa amri ya jeshi la polisi kuhusu kusitishwa kwa maandamano ya wagombea urais wakati wa uchukuaji fomu na kutafuta wadhamini haiwahusu wao.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alipozunguza na mwandishi wa gazeti la Nipashe.

Mwalimu alifafanua kuwa Ukawa hawafanyi maandamano bali watu wenyewe hujitokeza kwa wingi kuwapokea wagombea wao. Kwa kuzingatia hilo, alisema mapokezi ya kumtambulisha Lowassa yatafanyika mikoni kama kawaida.

Juzi, Jeshi la Polisi lilitoa amri ya kuzuia maandamano yoyote yanayofanywa na wafuasi wa wagombea urais wakati wa uchukuaji fomu na urudishaji fomu pamoja na zoezi la kusaka wadhamini mikoani.

Kauli ya Jeshi la Polisi iliyotelewa na Inspecta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki jijini Dar es Salaam ilifafanua kuwa uamuzi huo umechukuliwa kwa sababu za kiusalama na kuondoa usumbufu unaojitokeza kwa wananchi wakati wa maandamano hayo.

Jana, maelfu ya wakazi wa jiji la Mbeya walijitokeza kumpokea Edward Lowassa na kuambatana nae hadi katika viwanja vya Ruanda jijini humo ambapo alifanya mkutano mkubwa katika hali ya Amani na usalama huku polisi wakisaidia kuimarisha ulinzi.

Purukushani Za Uchaguzi Wa Tefa
Lowassa Aahidi Makubwa Mbeya, ‘Wahujumu’ Kukiona Cha Moto