Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) inayoundwa na vyama vikuu vya upinzani nchini umeanza rasmi jitihada za kumpata mgombea mmoja ataekuwa jembe litakalowawezesha kupata nafasi ya urais wa Tanzania dhidi ya CCM.

Viongozi wa vyama hivyo vya NCCR- Mageuzi, Chadema na Chama cha Wananchi (CUF) pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu wa chama hicho walikutana juzi jijini Dar es Salaam kujadili mgawanyo wa majimbo na mgombea wa kuwawakilisha kugombea urais kipenga kitakapopulizwa Oktoba mwaka huu.

Kikao hicho kilidumu kwa muda wa zaidi ya saa 12, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 6 na nusu usiku, kilimalizika bila kuwa na kauli ya kuueleza umma yaliyojili katika mjadala huo mrefu. Vyanzo vimeeleza kuwa mkutano huo ulimalizika bila kufikia muafaka wa pamoja.

Kwa mujibu wa chanzo, vutankuvute ilikuwa kumchagua mmoja kati ya mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wilbroad Slaa (Chadema).

“Wapo wanaong’ang’ania Lipumba agombee kwa upande wa Jamhuri ya Muungano na upande mwingne wanataka Dr. Slaa agombee huku na CUF wabaki Zanzibar,” kilieleza chanzo cha gazeti la Mtanzania.

Urais CCM: Majina Matano Haya Hapa, Dr. Nchimbi Apinga Uamuzi
Sikiliza/Download Wimbo Mpya Wa Barakah Da Prince Ft. Ruby - ‘Vumilia’