Vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi (Ukawa) vimepinga rasmi matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Twaweza huku wakibainisha mapungufu makubwa katika utafiti huo.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema kuwa taasisi hiyo ya Twaweza ilitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kueneza propaganda ya kukisaidia chama hicho ili kuwachanganya wananchi.

“Tafiti za kimataifa zinaonesha Lowassa atashinda kwa asilimia 74, watafiti wa humu ndani ambao ni wataalamu kwelikweli na ‘credible’ wametuonesha asilimia 76, online imetuonesha asilimia 79,” alisema Mbatia. “Sasa unaweza kuziunganisha hizo zote na tafiti za Twaweza ambazo hata mtoto mdogo unaona hiki ni kichekesho,” aliongeza.

Aidha, Mbatia alieleza kuwa utafiti wa Twaweza ulilenga katika kuwahadaa watanzania kwa kuipendelea CCM na kuwadhalilisha wagombea wa vyama vingine.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alieleza kuwa utafiti wa Twaweza unalenga katika kukipendelea chama cha mapinduzi na haukuwa wa kitaalamu kwa kuwa sampuli iliyotumika ni ya kundi la watu waliowachaguliwa lilikuwa limepangwa.

“Twaweza wana kundi lao la watu wao ambao ndio waliowapigia simu huwa wanawatumia watu walewale, sio kama walichagua namba za simu ‘randomly’ na kupiga simu kuwauliza, waliwapigia watu walioko kwenye hilo kundi lao na kuwauliza maswali,” alisema Profesa Baregu.

Viongozi hao wa Ukawa walieleza kuwa Twaweza wamewadhalilisha wagombea wa vyama vingine kwa kuwaweka katika kipengele bubu kilichotajwa kama ‘Vingine’.

Kikwete Azungumzia Kauli Za Magufuli Kuikosoa Serikali Yake
NEC Yabariki Kauli Za Bulembo kuhusu Ikulu