Siku moja baada ya CCM kumpata mgombea wa kiti cha urais ambaye ni waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, joto limehamia upande wa pili ambao ni vyama vya wapinzani.

UKAWA inayoundwa na umoja wa vyama vikuu vya upinzani nchini umemaliza vikao vya ndani na mijadala kuhusu nani atakayesimama kugombea nafasi ya urais. Chama hicho kinatarajia kutangaza rasmi jina la mgombea huyo kesho, Julai 14.

Akiongea na BBC, Mwenyekiti Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa umoja huo umepanga kumtangaza mgombea wake kesho na kwamba mjadala wa kugawana majimbo ya ubunge 211 umeendelea vizuri na umekamilika kwa asilimia 90.
Taarifa za awali kutoka katika vikao hivyo zimeeleza kuwa chama hicho kimemchagua Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wilbroad Slaa kugombea nafasi hiyo.

UKAWA inaundwa na Chama Cha Wananchi (CUF), NCCR- Mageuzi na Chadema.

Lulu Aielezea Post Yake Tata Kuhusu Urembo Na ‘Viti Maalum’
January Makamba: Magufuli Atarejesha Imani Kwa CCM