Uchaguzi wa Naibu Meya wa jiji la Dar es salaam, umefanyika ambapo wajumbe wa Baraza hilo wamekubaliana kwa kauli moja kuwa na Manaibu wa wili kutoka Chama Cha Wananchi (CUF) na mwingine Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hatua hiyo imetokana na kuwepo kwa idadi sawa ya wajumbe kwa pande zote mbili ambapo UKAWA ulikuwa na wajumbe 12 huku CCM ikiwa na wajumbe 12.
Akizungumza wakati wakutangaza uamuzi huo ulioafikiwa na wajumbe wa baraza hilo, Mstahiki Meya Isaya Mwita amesema kuwa kutokana na hali hiyo kila mmoja ataongoza kwa kipindi cha miezi mitatu hadi Juni 30 mwaka 2019.
“Tumefikia uamuzi huo kwani viongozi wamechaguliwa kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananchi bila kujali vyama vyao, kuwepo kwa viongozi wa vyama viwili tofauti haitawakosesha wananchi maendeleo kwakuwa wote wamechaguliwa kwa lengo la kuwatumikia wakazi wa jijini hapa,”amesema Meya wa Jiji Isaya Mwita
Hata hivyo, kabla ya kufanyika kwa maamuzi hayo, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta alitoa hoja baada ya kuwepo kwa mvutano mkali kuwa baraza lijigeuze kamati ili kufanya maamuzi ambayo yatakuwa na maslahi kwa wananchi kuliko kuendelea na mabishano.
-
Video: Membe atua usiku kikachero, Lowasa afunguka hatima yake Chadema
-
JPM ampa shavu Msekwa na wastaafu wengine watano
-
TCAA yajipanga kufanya majaribio ya mfumo wa Rada