Watu wengi hawana elimu juu ya vitu gani ambavyo huchagiza kwa asilimia nyingi magonjwa yasiyoambukiza kama ugonjwa wa moyo, kisukari, msukumo wa damu na n.k ambayo kwa karne hii yanasababisha vifo vya mamilioni ya watu, tena vifo vya ghafla.
Hivyo basi ili kujiepusha na magonjwa kama hayo hasa ugonjwa wa moyo ambao siku hizi huwapata watu wa rika zote, kiafya inashauriwa kila siku kufanya mambo 7 yafuatayo.
- Haishauriwi kuvuta sigara, ili kujikinga na magonjwa ya moyo, uvutaji wa sigara huchagiza kwa asilimia kubwa magonjwa ya moyo na kansa kutokana na moshi wenye kemikali unaoenda kuharibu mapafu, kifua na kufanya moyo kutanuka, hivyo kujiepusha na madhara hayo ni vyema kujiweka mbali na uvutaji wa Sigara.
- Kujamiana kimapenzi, hii ni maalumu kwa walio na umri juu ya miaka 18 ambapo madaktari wamefanya tafiti zao na kubaini kuwa tendo la kujamiana lina faida kubwa ya kuweka moyo wako katika hali ya usalama, kwani tendo hilo hupunguza homoni za furaha na kukufanya uweze kupunguza msongo wa mawazo kwani msongo wa mawazao kwa asilimia kubwa huchagiza magonjwa ya moyo.
- Inashauriwa kutumia glasi ya mvinyo wa zabibu (red wine), ila itumiwe kwa kiwango maalumu kwani kiwango cha wastani cha pombe yenye kilevi husaidia kuyeyusha mafuta mwilini na kukufanya mwili uwe na kiwango kizuri cha mafuta mwilini, kwani wingi wa mafuta mwilini husababisha magonjwa ya moyo.
- Punguza kiwango cha kutumia chumvi, Jopo la madaktari limebaini na kushauri kuwa kwa siku mtu anatakiwa kutumia kiasi kidogo cha chumvi kwa kutumia kipimo cha kijiko kidogo cha chai, kwani tafiti zimeonesha kuwa watu wanaotumia kiwango kikubwa cha chumvi hudhurika na magonjwa ya moyo.
- Inashauriwa kutumia chokolate nyeusi, yaani kipande kimoja cha chokolate kwa siku kwani husaidia katika kuweka sawa afya ya moyo wako kutokana na virutubisho kisayansi vinavyojulikana kama Antioxidants na flavonoids.
- Jizuie kutumia lifti, badala yake tumia ngazi, ofisi nyingi ni ghorofa hivyo watumiaji wa ofisi hizo hupendelea kutumia lifti, hivyo madaktari wanashauri kwa afya ya moyo wako ni vyema kutumia ngazi ili kuweka mapigo ya moyo wako sawa na kufanya mazoezi na kwa kufanya hivi si lazima kwenda mazoezini kwani kupanda ngazi ni zoezi tosha.
- Zingatia matunzo bora ya kinywa chako, Tafiti mbalimbali zimebainisha kuwa matunzo mabovu ya kinywa yanahusha moja kwa moja kusababisha magonjwa ya moyo, hivyo inashauriwa kusafisha kinywa mara kwa mara ili kuua bakteria na vijidudu vinavyotengenezwa kinywani.