Kupitia mitandao ya kijamii upande wa burudani moto moto za leo tarehe 13 ni kuhusu sherehe ya pili ya mtoto wa mwanamuziki Diamond Platinumz na mwanamitindo Hamisa Mobeto, Dylan au Abdul maarufu kama  4O’s.

Ambapo kwa mara ya kwanza kufanyika kwa sherehe hiyo baba mzazi wa Dylan, yaani Diamond Platinumz hakuhudhuria hivyo inasemekana kuwa sherehe hii ya pili imeandaliwa maalumu kwa ajili yake.

Mpaka sasa mwanamitindo Hamisa Mobeto hajazungumza lolote kuhusiana na shughuli hiyo na kueleza sababu za  kuifanya shughuli ambayo ilishafanywa siku zilizopita.

Aidha mashabiki wa staa huyo Hamisa Mobeto wameingilia kati swala hilo na kutupia jicho la tatu na kushauri kuwa Hamisa anahitaji mtu wa karibu kumpa ushauri wa kina.

Mashabiki wamehoji kuwa kulikuwa hakuna sababu ya kufanyika kwa sherehe hiyo ilihali kuwa ilishafanyika siku zilizopita.

Wengi wameeleza kuwa fedha hizo zingemsaidia kutengeneza maisha ya baadae ya mtoto wake kuliko kufanya mambo ya kidunia ambayo hupita kama upepo.

Klopp kuendeleza rekodi kumpiga Mourinho?
George Weah aongoza kwa kura za awali Liberia