Mwanamitindo na mjasiriamali maarufu wa nchini Kenya Huddah Monroe ameweka wazi kuwa yuko tayari kuwa mama ikiwa mwanamume anayetamani kupata naye watoto yuko tayari kuweka mezani kitita cha $1, 000, 000 ambazo ni sawa na zaidi ya Bilioni mbili za Kitanzania.
“Nauza tumbo langu. Lol! $1, 000, 000 (KSh113, 150, 000) ili niwe mama wa mtoto wako mchanga, Kuhusu Msaada wa mtoto tutakubalina wakati wa kushiriki tendo ili kupata mimba,” alisema Huddah Monroe.
Mnamo mwaka 2020, Hudda alikiri kwamba kamwe hatoweza kumhifadhi kwenye tumbo lake mtoto wa mwanamume fukara, bila kujali hali.
Kupitia kwenye Insta story yake, Huddah alisema kwamba katu, hatoweza kukubali kupata mtoto wa mwanamume asiye na uwezo wa kifedha kwa sababu hiyo ni sawa na kumleta mjinga hapa duniani hali ya kuwa unajua.
Licha ya kuweka hilo wazi pia alionyesha kushangazwa na hata kwa nini baadhi ya wanawake wanakubali kushika mimba za wanaume wa namna hiyo.
“Siwezi kuleta mjinga katika ulimwengu huu kwa kujua! Mungu aniepuashie!”
Huddah aliongeza huku akijikita katika kuwashauri wafuasi wake kwenye mtandao wa Instagram kuwa kila wakati ni vyema kuzingatia kile kinachoweza kukuletea furahisha na kupuuza maoni ya wengine huko mitandaoni.
“Katika maisha, Daima jikite kwenye kitu kinachokufanya uwe na furaha! Achana na kile mtu yeyote anafikiria kuhusu wewe.” Aliandika.
Huddah amekuwa si mwenye kuogopa kuweka mitazamo yake hadharani kupita ukurasa wake wa mtandao wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya Milioni 2 bula hofu ya kuhukumiwa na jamii juu ya mambo mbalu mbali ya kustaajabisha ambayo amekuwa akishiriki kwenye mtandao huo.