Ukraine imesema imechukua udhibiti wa eneo zima la Kyiv baada ya wanajeshi wa Urusi kurudi nyuma kutoka katika baadhi ya miji muhimu karibu na mji huo mkuu.

Naibu waziri wa ulinzi Ganna Maliar ameandika kwenye ukurasa wa Facebook ambapo ameandika kuwa miji ya Irpin, Bucha, Gostomel na eneo zima la Kyiv imekombolewa kutoka kwa mvamizi.

Miji hiyo ilikuwa imeharibiwa vibaya kutokana na mapigano na raia wengi waliuawa.

Meya wa miji hiyo amesema watu 280 walizikwa katika kaburi la pamoja katika mji wa Bucha na miili mignine ikiwa imesambaa kwenye mji huo huku mamlaka zikisema karibu watu 200 waliuawa katika mji wa Irpin tangu Urusi ilipoivamia Ukraine.

Ukraine imesema askari wa Urusi wanaondoka kwenye maeneo ya kaskazini na wanaonekana kujielekeza zaidi upande wa mashariki na kusini mwa Ukraine. 

TRA kuanza kutumia mfumo wa kieletroniki kuanzia mwezi huu
TMA yamtunuku Rais Samia tuzo ya heshima