Ukwaju ni tunda maarufu sana ambalo hupatikana katika maeneo yenye uoto wa kitropiki. Kwa kingereza hujulikana kama tamarind, na kwa kitaalamu (botanical name) huitwa tamarindus indica, waarabu huita tamru alhind ambapo katika baadhi ya maeneo hutumiwa kama kiungo katika mboga.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya kila gramu 100 za ukwaju kuna 36%za thiamin, 35% Iron, 23% magnesium ,na 16%phosphoras, pia ukwaju una kiwango kikubwa cha tartic acid Ma citric acid.

Zifuatazo n faida za ukaju katika mwili wa Binadamu.

Husaidia kuongeza uwezo wa macho kuona (improving eyesight), Matumizi ya ukwaju kwa kula au kutumia kama juisi huondoa matatizo ya macho na kukufanya uwe na macho yenye afya.

Husaidia kwa wenye shinikizo la damu unashauriwa kunywa juisi ya ukwaju Mara kwa mara kwasababu ukwaju hupunguza kiwango kikubwa cha lehemu mwilini (cholesterol).

Huondoa tatizo la nywele kukatika, na kuzipa mng’aro halisi, chemsha ukwaju, kisha tumia maji yake, changanya na vijiko viwili vya bizari, oshea nywele zako. Kisha ziache nusu saa na uzioshe kwa maji ya vuguvugu.

Maajabu ya kituungu saumu kwa wanaume
Jafo atoa siku 10 usajili miradi