Kama ulikua unafikiri unene wa kupindukia upo kwa Bin – Adamu pekee basi umegonga mwamba, kwani wapo wanyama wenye unene uliopitiliza pia.

Katika Jimbo la Virginia nchini Marekani, moja ya camp za makazi ya wanyama, kuna Paka mnene zaidi duniani ambaye anafahamika kwa jina la Patches ambaye anaingia katika rekodi za dunia za Guinness.

Kutokana na uzito huo, mamlaka zimeamua kumfanyia diet na wanasema tayari wamefanikiwa kumpunguza kilo mbili (kutoka 40 alizokuwa nazo hadi 38 kwasasa).

Madaktari wa mifugo wanasema uzito wa wastani wa paka hautakiwi uzidi kilo 10 na Wasimamizi za camp hiyo wanasema sababu kuu ya paka huyo kuwa na uzito wa kupitiliza ni ulafi.

Fadhili Majiha kumsindikiza Mfaume Mfaume
Erling Haaland alikoroga Manchester City