Tunda la papai, majani na utomvu wa mmea huu hutumiwa kutengenezea dawa maeneo mbalimbali duniani, vilevile, matunda na utomvu wake hutumika kutengeneza pombe na mvinyo katika baadhi ya nchi, huku wengine wakitumia mpapai kutengenezea dawa kwa ajili ya mifugo na binadamu.

Ulaji wa antioxidanti zilizopo kwenye papai mfano beta-carotene husaidia katika kupunguza athari za kupata maradhi ya saratani kwa vijana. Ulaji wa tunda hili husaidia katika kudhibiti upatikanaji wa saratani kwenye via vya uzazi hasa saratani ya korodani.

Punje za papai ni dawa kwa baadhi ya matatizo ya ini na figo, Pia kwenye papai kuna protelytic enzymes hii husaidia katika kuuwa bakteria na minyoo pamoja na wadudu wengine hatari ndani ya tumbo (mfumo wa kumeng’enya chakula).

Papai linatambulika kwa kuwa na uwezo wa kuulinda mwili na maradhi ya uzee kama macho, misuli na kuzeheka kwa haraka. Ndani ya papai kuna Zeaxanthin hii ni anti oxidant ambayo inakazi ya kuchuja miale hatari ya jua, inaaminika kuwa antioxidant hizi husaidia katika afya ya macho na husaidia katika kudhibiti kudhoofu kwa misuli.

Ulaji wa tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya mifupa na kudhibiti kupasuka kwa mifupa. Vitamin k vilevile husaidia katika ufyonzwaji wa madini ya calcium na huzuia upotevu wa madini haya kupitia mkojo, kumbuka madini haya pia ni muhimu katika kuimarisha na kudhibiti afya ya mifupa.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 9, 2020
Ahadi ya Joe Biden kwa wamarekani