Serikali nchini, imewaasa Wadau wa sekta za Mifugo na Uvuvi kujisajili na kushiriki vyema katika Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika 2023 – AGRF, unaotarajia kufanyika Septemba 5-8, 2023 ili waweze kufungua fursa za kibiashara.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameyabainisha hayo katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane), jijini Mbeya na kusema tayari Wizara inafanya jitihada kuhamasisha wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kushiriki katika mkutano huo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wapili kutoka kushoto) akiangalia baadhi ya mifugo iliyopo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya). Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi. 

Mhe. Ulega amesema mkutano huo wa Afrika utakaofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 3,000 wa ndani na nje ya nchi, unatarajia kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi na kuongeza wigo wa mawasiliano ya kibiashara kwa wadau wote.

Kuhusu Programu ya Kielelezo “Jenga Kesho Iliyo Bora” BBT – LIFE kwa ajili ya kuwezesha vijana kupata elimu ya vitendo katika unenepeshaji wa mifugo na viumbe vya kwenye maji, Waziri Ulega amesema hadi sasa takriban vijana 240 wapo kwenye mafunzo.

Tutengeneze hatma njema ya Wazanzibari - Juma Duni
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 7, 2023