Mshambuliaji wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo,Thomasi Ulimwengu amesema kuwa kufanya vibaya kwa klabu hiyo katika ligi ya mabingwa msimu huu ni upepo mbovu hukua akiamini kuwa msimu ujao mambo yatakuwa mazuri.

TP Mazembe katika michuano ya ligi ya Mabingwa msimu huu wakiwa katika kundi B wanakamata nafasi ya mwisho nyuma ya timu za Mamelod Sundowns, CR Belouizdad na Al Hilal.

Ulimwengu alisema kuwa katika mpira wa miguu timu kubwa nyingi ambazo zimekuwa zikifanya vizuri kama ilivyozoeleka huteleza na kupitia upepo mbaya jambo ambalo anaamini halitajitokeza tena katika msimu ujao wa ligi hiyo.

“Msimu huu tumefanya vibaya kila mtu ameona lakini si mara ya kwanza katika mpira wa miguu kwa timu bora na kubwa kama Mazembe kufanya vibaya,kwetu tunaamini ulikuwa ni upepo mbaya kama ambavyo huzikuta timu nyingine kubwa na bora kushindwa kufanya vizuri.

“Msimu ujao naamini mambo yatakuwa mazuri kwetu na tutafanya vizuri katika michuano hii kuliko ilivyokuwa msimu huu,najua haitakuwa kazi ndogo lakini tutahakikisha hili halijitokezi,”alisema mshambuliaji huyo.

Ndumbaro kushughulikia makazi hifadhi ya Ngorongoro
Mayay: Hawa jamaa ni hatari kwa sasa