Jukumu la Ulinzi na Usalama katika Bandari ya Dar es Salaam litaendela kusimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama ambavyo vipo katika maeneo yote ya Bandari kwa kuzingatia Sheria za nchi na mikataba ya kimataifa.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa na kuongeza kuwa suala hilo limezingatiwa pia katika Mkataba wa IGA na kuwekwa bayana kwamba masuala ya Ulinzi na
Usalama hayatakiukwa kwa namna yeyote wakati wa utekelezaji shughuli za uwekezaji.
Amesema, “Vilevile, taasisi zote za Serikali ambazo zinahusika katika shughuli za bandarin zitaendelea kutekeleza majukumu yao kwa mujibu Sheria ndani ya eneo la bandari.”
Aidha, amebainisha kuwa uwepo wa sekta binafsi kutoa huduma katika maeneo ya bandari umeendelea kuwepo na kusimamiwa na Serikali kwa miongo tofauti tofauti. Aidha, katika kipindi chote ambacho Sekta Binafsi imehusishwa katika uendeshaji wa bandari, hakujawahi kujitokeza tukio la kuhatarisha usalama wa nchi.