Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP. David Misime amesema kuwa Jeshi la polisi litahakikisha ulinzi na usalama unaimarika kabla, wakati na baada ya maonesho ya sabasaba yanayofanyika Jijini Dar es Salaam ili wageni, washiriki wa ndani na wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu na zoezi hilo ni kwa maeneo yote ya nchi.
SACP Misime ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau wengine hususan vyombo vya ulinzi na usalama na wasimamizi wa maonesho Tantrade kuhakikisha kuna hali ya utulivu na amani.
Amesema, “ukitaka nchi iwe na amaendeleo makubwa lazima uhakikishe kwamba swala la ulinzi na usalama kwamba linakuwa kwa la hali ya juu na ili uweze kuwa na hali hiyo ya juu ya ulinzi na usalama na utulizvu na amani lazima utumie silaha muhimu sana katika kubaini na kuzuia uhalifu aambayo ni elimu kwa mwananchi.”
Akizungumzia elimu inayotolewa na Jeshi hilo kuhusu mambo mbalimbali ya usalama katika maonesho hayo, Misime amesema ““katika banda la Polisi tunatoa elimu hivi sasa duniani kote majeshi yote ya polisi yanajikita katika swala la utoaji elimu kwa wananchi wake ili waweze kushirikiana na jesh la polisi katika kubaini na kuzuia uhalifu.”
“ukimpa elimu atajitambua yeye na kwamba thamani yake ni nini na anahitaji kuwa salama na kama anataka kufanya shughuli zake katika mazigira ya amani,“ aliongeza Misime.
Hata hivyo, ameongeza kuwa mwananchi anapopata ufahamu juu ya madhara ya uhalifu ataweza kushirikiana na jeshi la polisi katika kubaini na kuzuia uhalifu, na kinachoangaliwa zaidi ni kuzuia na si kupambana kwasababu gharama za kupambana ni kubwa.