Eva Godwin – Dodoma.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amesema licha ya Tanzania kuingia katika uchumi wa kati, lakini bado zinahitajika jitihada za ziada, ili kuwainua wananchi dhidi ya umasikini na hasa wale waishio vijijini.

Pinda ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mkakati wa miaka mitano wa kuimarisha masoko ya mazao ya kilimo nchini Tanzania, huku akizitaka Sekta na Wizara husika kupambana na umaskini wa kipato na kuipa nafuu mifumo ya chakula.

MATUKIO @ MICHUZI BLOG: ZIARA YA WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA SONGEA MJINI

Amesema, “pamoja na mambo mengine lengo ni kubadilisha mifumo ya kilimo nchini Tanzania sambamba na kuongeza tija na kipato kwa wakulima wadogo maana licha ya kuingia katika uchumi wa kati, lakini bado tunahitaji kuwainua wananchi.”

Mapema hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo Duniani – UNDP, liliripoti kuwa, licha ya nchi 25 kupunguza nusu ya umasikini ndani ya miaka 15, bado watu bilioni 1.1 wanasalia katika umasikini.

Madaktari Bingwa wa Ujerumani kuwasili Tanga kwa upasuaji
Azam FC yafafanua usajili wa Alassane Diao